Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Idara ya Kimataifa ya Hawza, kwa kuzingatia mabadiliko makubwa katika dunia ya kisasa, kuangalia uwezo wa kimkakati wa ulimwengu wa Mashariki, na katika mfumo wa masharti ya mpango wa pili wa miaka mitano wa Hawza, imeweka katika ajenda zake hatua za utekelezaji za kuunda uwezo na miundombinu inayohitajika kwa ajili ya kufanikisha dira na malengo ya mpango huu katika nchi za Asia ya Mashariki.
Kwa mujibu wa habari zilizopokelewa, ujumbe wa Kituo cha Usimamizi wa Hawza za Elimu ya Kiislamu, ukiwahusisha Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad-Reza Barteh na Muhammad-Sadiq Amin-Din, katika mikutano yao na shakhsia za kielimu, kitamaduni na vyuo vikuu, pamoja na viongozi wa dini wa eneo hilo, walijadili misingi ya ushirikiano wa pamoja na kusisitiza utekelezaji wa kivitendo wa makubaliano yaliyoafikiwa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Barteh, katika mazungumzo na mwandishi wa Hawza, huku akirejelea uwezo wa kifikra wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (Amani iwe juu yao) na urithi mkubwa wa ustaarabu wa Kiirani alieleza kuwa, ushirikiano wa kihistoria na uelewa wa pamoja kati ya Iran na Asia ya Mashariki ni mtaji muhimu kwa ajili ya kubuni ushirikiano wa siku zijazo.
Alitaja pia maandalizi ya lugha na mitazamo, maendeleo na malezi ya rasilimali watu, kuimarisha ufunguzi wa kifikra, pamoja na kupokea na kutuma ujumbe wa wasomi kutoka pande zote mbili, kuwa ni miongoni mwa mahitaji ya kuunda mahusiano endelevu, ya kina na ya kudumu katika uwanja huu.
Hujjatul-Islam Amin-Din pia, akirejelea historia ya mawasiliano ya kitamaduni na kidini kati ya Iran na Asia ya Mashariki, alieleza kuwa; kinga ya kiasi katika eneo hili dhidi ya wimbi la chuki dhidi ya Uislamu ni fursa muhimu kwa ajili ya kupanua na kuinua mahusiano ya kielimu na kidini.
Inafaa kutajwa kuwa, kukuza na kuimarisha mahusiano ya kielimu, kitamaduni, kidini na kistaarabu kati ya Hawza za Elimu ya Kiislamu za Iran na nchi zilizopo Mashariki ni miongoni mwa malengo na vipengele vya mpango wa pili wa miaka mitano uliopendekezwa wa Hawza katika uwanja wa kimataifa.
Maoni yako